Burudani

Joh Makini: Tulipeni vizuri na tutafanya maajabu jukwaani

Joh Makini alizikonga nyoyo za mashabiki wa hip hop Jumamosi iliyopita kwenye show ya P-Square, lakini anaamini kuwa yeye na wasanii wengine wa Tanzania, wanaweza kufanya maajabu zaidi kama wakipewa malipo mazuri.

Joh Makini

Akiongea na tovuti ya Times FM, Mwamba wa Kaskazini alisema P-Square wanajituma jukwaani kwasababu wanalipwa vizuri.

“Performance yao ilikuwa nzuri lakini naamini kwamba tunaweza kufanya bigger than that kama tukiwezeshwa vizuri financially,” Joh aliiamboa tovuti hiyo.

“Kwa hiyo sijashangaa, yaani hawajafanya kitu cha kunishangaza kwa kuwa naamini kwamba wanalipwa vizuri. kwahiyo walistahili kufanya kile kitu walichokifanya kutokana na jinsi ambavyo wanapewa treatment kama wasanii wa kimataifa. Na nilitarajia labda watafanya hata zaidi ya kile ambacho nilikiona kutokana na treatment ambayo wanapewa kama International artists.

Kwa hiyo nilichokiona pale ni kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi ya tulivyofanya, ama hata zaidi ya wasanii wengi wa kimataifa kama tutawezeshwa,” aliongeza rapper huyo.

Source: Times FM website

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents