Michezo

Johanna Konta afukuzia nyota ya Maria Sharapova

Mchezaji tenis raia wa Uingereza, Johanna Konta amesema kuwa kocha wake wa sasa, Michael Joyce anauwezo wa kumuwezesha kutwaa taji la Grand Slam.

Joyce, ambae ni maarufu na mwenye mafanikio makubwa katika kazi hiyo ya ukocha baada ya kumfundisha bingwa mara tano wa taji la Grand Slam, Maria Sharapova amethibitishwa wiki iliyopita kuingia kandarasi ya kumnoa Muingereza huyo anaeshikilia nafasi ya nne katika viwango vya mchezo tenis duniani.

“Nafikiri nilipoteza kiwango changu kwa kiasi chake hasa mwishoni mwa msimu huu,” amesema Konta.

Konta ameongeza “Nadhani nipo imara na tayari kuelekea katika muelekeo ambaonaona nitakuwa na maendeleo na hivyo nasubiri kuona ikitokea.”

“Nahitaji kuona napiga hatua na nikizidi kupata uzoefu ili niweze kuwa bora naninaeweza kucheza michuano mikubwa. Kapata nafasi ya kufanya kazi na Michael nimoja ya hatua ya kuelekea katika mafanikio.”

Kitendo cha Johanna Konta kumpatia kandarasi kocha Michael Joyce ambae amempatia mafanikio makubwa mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani, Maria Yuryevna Sharapova kinatafsriwa kama kufukuzia mafanikio aliyopata Sharapova.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents