Aisee DSTV!

John Bocco aongeza kandarasi kwa mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba, mkataba wake sasa kufika tamati 2021

Mchezaji wa klabu ya Simba, John Bocco ameanguka saini ya mkataba wake mpya wa miaka miwili dhidi ya miamba hiyo ya soka ya Tanzania na Mabingwa wa ligi kuu.

 

Kupitia akaunti yao ya Instagram, Simba imeanika wazi utiwaji saini wa nahodha wa timu hiyo ambao sasa uutamuweka hapo mpaka mwaka 2021.

”John Bocco amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu yetu. Bocco ambaye alikuwa mchezaji bora wa Simba na Ligi Kuu kwa msimu wa 2017/18 na Mshambuliaji Bora kwa msimu wa 2018/19 amefunga jumla ya mabao 30 ya Ligi katika misimu miwili. #NguvuMoja .”

https://www.instagram.com/p/ByhzrClHxkH/

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW