John Cena ampigia saluti muigizaji wa filamu maarufu zaidi duniani, Shah Rukh Khan

Mwanamieleka maarufu zaidi duniani, John Cena huenda akawa ni moja wa mashabiki wakubwa wa Muigizaji kutoka Bollywood, Shah Rukh Khan hii kutokana na Mara kwa mara kutumia nukuu za mkali huyo wa filamu za kihindi.

Image result for john cena
John Cena

John Cena ametumia nukuu ya Muigizaji huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuonesha hisia zake na kisha kumshukuru mkali huyo wa filamu.

Kazi zako na Maneno yako yanawafikia watu wengi sana, yananifanya niwe na tabasamu muda wote, niwe na furaha na kukua kila siku. Ahsante Sana kwa kupata mtu Kama wewe.“ameandika John Cena.

Naye, Khan kupitia ukurasa wake wa Twitter amepokea pongezi hizo kwa kumjibu “nashukuru Sana rafiki yangu kwa kusambaza vitu vizuri. Sisi Kama sote ni watu maarufu tunatakiwa tufanye kazi nzuri ili kuwashawishi watoto wanaotutazama

Khan anatajwa na jarida la Forbes kuwa ni Muigizaji wa pili wa filamu kuwa na mkwanja mrefu zaidi duniani anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni $740 sawa na tsh trilioni 1.6 .

Baadhi ya mastaa nchini Tanzania akiwemo Diamond Platnumz ni moja ya watu waliowahi kuweka wazi kuwa wanavutiwa sana na kazi za Khan.

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW