Tragedy

John Mjema ajiua kwa kisu

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya, John Mjema ‘Bomba la Mvua’, juzi jioni alifariki dunia baada ya kujichoma kisu mwenyewe sehemu ya shingo, imefahamika.

na Nuru Yanga

 

 

 

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya, John Mjema ‘Bomba la Mvua’, juzi jioni alifariki dunia baada ya kujichoma kisu mwenyewe sehemu ya shingo, imefahamika.

 

Akithibitisha kifo cha msanii huyo aliyewahi kutamba na vibao kadhaa kikiwamo kibao cha ‘Wachumba 30’, Mjema aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili kwa muda mrefu, alikumbwa na mauti papo hapo.

 

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu ambaye hata hivyo hakupenda kutajwa jina lake kwa sababu mbalimbali, hadi anakutwa na tukio hilo alikuwa akiishi Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam, huku akiwa anasumbuliwa na tatizo la akili.

 

Msemaji huyo alisema siku hiyo ya tukio, Mjema alijichoma kisu shingoni na kufariki dunia papo hapo.

 

“Mjema ni ndugu yangu, amefariki jana jioni (juzi) papo hapo baada ya kujichoma kisu shingoni na ninapozungumza nawe, taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika na kesho tutakuwa na jibu sahihi kwamba atazikwa wapi na lini,” alisema ndugu huyo.

 

Kabla ya kupatwa na maradhi ya akili, Mjema amewahi kutamba na vibao mbalimbali, vikiwamo ‘Wachumba 30’ na ‘Mimi si Mwizi’, alizowashirikisha wasanii wengine, akiwemo Steve 2K, ambaye alidaiwa kufariki dunia kwa kuchomwa kisu akitoka disko.

 

Kibao kingine kilichowahi kumng’arisha Mjema ni ‘Shani’, alichomshirikisha Spider.

 

Mjema alikuwa mmoja wa wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Mambo Poa, lililokuwa likiundwa na wasanii watatu, ambao ni marehemu Mjema, Spider na Steve 2K (pia marehemu).

 

Mbali ya muziki, katika maisha yake Mjema alishawahi kuwa mtumishi wa serikali katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi, hazikuzaa matunda.

 

 

 

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents