Michezo

John Terry: Bado sifanya mawasiliano na timu kujua hatma yangu

Nahodha wa Chelsea John Terry amesema hadi saivi bado hajafanya mazungumzo na klabu yake hiyo kuhusu mkataba mpya licha ya kocha Guus Hiddink, kusema huenda mchezaji huyo akabaki katika kikosi hicho.

30F9E3F600000578-0-image-a-9_1454874738137

Wiki iliyopita mchezaji huyu alieleza bado hajapewa ofa mpya huku mkataba wake ukiwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi dhidi ya Manchester united, amesema “nimeweka wazi nataka kubaki hapa, japo ni ngumu timu ndio kitu muhimu zaidi na hakuna mawasiliano kati yangu na timu kwa sasa.

Terry alijiunga na timu ya vijana ya Chelsea mwaka 1995, amecheza jumla ya michezo 478 ya ligi kuu ya England. Na kumekua na tetesi anaweza kwenda nchini Qatar katika timu ya Al Arabi, kungana na mchezaji mwenzake wa zamani Gianfranco Zola, ambae ni kocha wa kikosi hicho.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents