Burudani

Jokate amtaja mchezaji anayemkubali kati ya Ronaldo na Messi

By  | 

Licha ya Jokate Mwegelo kuwa karibu na mitindo na kujikita zaidi kwenye siasa na biashara, lakini pia mrembo huyo ni mfatiliaji wa karibu wa mchezo wa soka.

Jojo ameshawahi mara kadhaa kuthibitisha kuwa ni shabiki wa Arsenal, lakini hakuwahi kumtaja ni mchezaji gani ambaye anamkubali zaidi kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Unafikiria anamkubali nani kati ya hao?

Basi mrembo huyo kupitia mtandao wa Instagram, ameweka picha hiyo hapa chini na ameonyesha kuwa anamkubali zaidi Ronaldo tena amedai mchezaji huyo anakipaji zaidi kuliko Messi.

“Ukichana na kuwa Arsenal dam dam pia niko hapa CR7 kipaji kuliko Messi. 🙈🙌🏽,” ameandika Jokate.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments