Promotion

Jokate, Salama, Wolper kuwa wageni maalum kwenye show ya wanafunzi ‘Jitambue’ Dec 7, wasanii 15 kutumbuiza

Jokate Mwegelo, Salama Jabir, Jacqueline Wolper na Steve Nyerere wanatarajiwa kuwa wageni maalum kwenye show ya wanafunzi wa sekondari jijini Dar es Salaam iliyopewa jina ‘Jitambue’ na iliyoandaliwa na kampuni ya Urban Fresh.

urban 4 A

Show hiyo itafanyika December 7, Kenton Hgh School jijini Dar es Salaam. Mastaa hao wanne watazungumza mbele ya wanafunzi masuala mbalimbali yatakayowasaidia kujitambua.

Pia kutakuwa na burudani kali kutoka wasanii zaidi ya 15 ambao ni pamoja na Young D, Godzilla, Young Killa, Richie Mavoko, Madee, Country Boy, Wakazi, Gosby, Mabeste, M-Rap, Walter Chilambo, Cindy Rulz, Damian Soul, Bob Junior na wengine.

Show itaanza saa nne 4 asubuhi hadi saa 1 usiku kwa kiingilio cha shilingi 5,000. Usikose.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents