Michezo

Jonas Mkude apata mrithi Simba SC

Benchi la ufundi la klabu ya Simba likiwa chini ya Kocha Mkuu Mcameroon, Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu hiyo.

Beki wa kimataifa raia wa Zimbabwe, Method Mwanjale

Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu hiyo beki wa kimataifa raia wa Zimbabwe, Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa Simba SC akichukua nafasi inayo achwa na Jonas Mkude atakaesalia kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho ambacho kwa sasa kipo Eden Vale Johannesburg nchini Afrika Kusini kwaajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza mwezi ujao na michuano mbali mbali.

Kwenye mabadiliko hayo ambayo ni yakawaida benchi hilo la ufundi pia limemteua mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu, Mohammed Hussein (Tshabalala) na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents