Burudani

Jose Chameleone amshushia barua nzito Rais Museveni ya kumuomba amsamehe Bobi Wine ‘kukosolewa ni changamoto za uongozi’

Msanii mkongwe wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone amemuandikia barua Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wa kumuomba amsamehe rapa Bobi Wine ambaye pia ni Mbunge wa chama cha upinzani nchini humo.

Image result for Jose chameleone Bobi wine and museveni
Jose Chameleone na Bobi Wine

Katika barua hiyo, Chameleone amesema Rais Museveni ni kama baba wa taifa hilo na anapaswa kuwa na roho ya kusamehe kama vitabu vitakatifu vinavyosema huku akisistiza kuwa masuala ya kupishana kiitikadi kwenye siasa ni  changamoto tu kwenye kazi yasijenge uadui.

 

Letter to His Excellency President of the republic of Uganda.
Dear President,
Seeking appointment or going through protocol will not deliver my urgent letter to you. 

Right now I hope we all rather can let it be a temporary political mishap per what happened in the district of Arua on Monday. Unfortunately it left you car Vandalized,Many of us inconvenienced – A soul lost, And another Ugandan,brother, Friend,Fellow singer Honourable as appointed by Kyadondo east-Robert Kyagulanyi alias Bobi Wine and many counterparts in an unfortunate situation. Honourable Kyagulanyi has always collaborated with me and all of us society to free Uganda from
Foreign sounds,Sell our culture beyond borders through our capital ability – Music.
Bobi Wine has over time exhibited his leadership admiration. Just Like any young ambitious man, he has treaded a path of aggressiveness.
Your excellency,Our brother, Your son Bobi Wine could have gone wrong on execution of some of his ideologies. That’s a challenge .

As head of state and forefather, It’s a great one too to lead us in example of forgiveness and reconciliation as that is one of the prime problems that have hindered our society.We are so unforgiving.
I as a son of this nation on behalf of the slogan. “For God and my Country” With all honour beg you the President to symbolise forgiveness in such a time. We can all wrong but better the forgiver.Mr President, You are a Father,Parent and always forgiving one.We shall all remain calm and be hopeful that the coming developments will see us all live harmoniously and have a peaceful country henceforth.
JOHN: 8:7
Dialogue is the answer
For God and my country
🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬

Jose Chameleone.

Chameleone ameandika barua hiyo ikiwa ni siku chache zimepita tangu maofisa wa polisi mjini Arua wamkamate Rapa Bobi Wine kwa tuhuma za uchochezi kwenye kampeni za ubunge zinazoendelea mjini humo.

Siku ya Jumatatu Wakazi wa Arua waliupiga mawe msafara wa rais Museveni wakidai kuwa amelituma jeshi la polisi kumuua dereva wa Bobi Wine.

Mpaka sasa familia ya Bobi Wine inalalamika kwamba haijui sehemu aliyoko Mbunge huyo wa jimbo la Kyadondo Mashariki.

Jose Chameleone amemsihi Museveni kumuachilia huru Bobi Wine japo amekiri kuwa Bobi alifanya makossa, “Kwa heshima kuu nakuomba umsamehe Bobi Wine. Kila mtu anaweza akafanya kosa na hakuna kosa ambalo haliweza likasameheka”

Kulingana na taarifa za polisi ni kwamba Bobi Wine anapokea matibabu japo familia yake inadai kuwa Mbunge huyo alikuwa buheri wa afya wakati alipokamatwa.

SOMA ZAIDI – Raia wenye hasira waushambulia kwa mawe msafara wa Rais Museveni, Mbunge wa upinzani ‘Bobi Wine’ akamatwa kwa uchochezi

Imeandikwa na Moses Njoge

Related Articles

5 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents