Michezo

Jose Mourinho akataa dili nono la kuinoa klabu hii kubwa barani Ulaya

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amekataa ofa ya kuinoa klabu ya Benfica ya nchini kwao Ureno.

Kwa mujibu wa gazeti la AS, Jose Mourinho aliombwa kukinoa kikosi hicho ikiwa ni masaa machache yaliyopita baada ya kocha wa klabu ya Benfica Rui Vitoria kutimuliwa mapema jana Jumamosi Januari 05, 2019 .

Mourinho alishawahi kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Benfica miaka ya 2000 akiwa chini ya Jupp Heynckes.

Mourinho amekataa dili hilo katika kipindi hiki ambacho, klabu kubwa kama Real Madrid zikimuhitaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents