Michezo

Jose Mourinho akerwa na usajili wa Neymar

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Brazili, Neymar da Silva Santos Junior  kuhamia klabu ya Paris Saint-Germain umebadili kilakitu katika soko la wachezaji.

Paris Saint-Germain paid £198m to sign Neymar

Paris Saint-Germain imemsajii, Neymar kwa paundi milioni 222

Mourinho anaamini kuwa United imeokoa mamilioni ya fedha baada ya kufanya usajili wake mapema kabla ya usajili wa Neymar Jr kufanyika.

PSG ilifanikiwa kuweka rekodi ya dunia kwa kumsajili Neymar  kwa paundi milioni 222 na kuvunja rekodi iliyowekwa na United ya paundi milioni 89.3 ya kumsajili Paul Pogba katika majira ya joto.

Kisha kufuatiwa na Barcelona kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele kwa ada ya paundi milioni 97.

Ousmane Dembele could cost Barcelona up to £135m

Ousmane Dembele asajiliwa kwa ada ya paundi milioni 97

PSG ikafanya usajili mwingine mkubwa wa kushtukiza kwa mkopo wa muda mrefu mchezaji wa Monaco, Kylian Mbappe kabla ya kuingia mkataba naye wa paundi milioni 166.

PSG are expected to pay Monaco £166m for Kylian Mbappe next summer

Inaaminika PSG itailipa Monaco paundi milioni 166 kwa kinda wa Ufaransa, Kylian Mbappe msimu ujao

Kisha Manchester United kumsajili Romelu Lukaku kwa paundi milioni 90.

Hivyo Mourinho anaamini ameokoa kiasi kikubwa cha fedha baada ya kukamilisha usajili wake mapema mwezi Julai.

Jose Mourinho believes Man Utd 'did well' in the transfer market

Jose Mourinho anaamini Man Utd imefanya vizuri katika dirisha la usajili

“Nafikiri tulitumia akili sana, tulihisi kwamba kunakitu kitakuja kutokea kitakachobadili soko la wachezaji milele”, Mourinho alikiambia chombo cha habari cha The Times.

“Soko la usajili lilikuwa la kawaida hapo awali lakini msimu huu hali ni tofauti kabisa, Neymar amebadili kilakitu”.

“Naamini Lukaku kama ingekuwa tunamsajili Agosti 31 basi gharama yake ingefika paundi milioni 150, Matic angefika paundi milioni 60 hadi 70, hapa ndipo unapoona Neymar alivyobadilisha kila kitu”.

“Kama usajili wa Paul Pogba ungekuwa bado ndiyo unaoshikilia dunia basi Philippe Coutinho kwa sasa angeuzwa kwa paundi milioni 101 kwenda Barcelona”.

“Watu sasa wanatazama paundi milioni 200 ndiyomaana mchezaji wa paundi milioni 20 anakuwa paundi milioni 40, mchezaji wa gharama ya paundi milioni 40 anakuwa paundi milioni 60 kila kitu kimebadilika”.

Mourinho says Lukaku would have cost £150m on Deadline Day

Mourinho anaamini Lukaku angegharimu paundi milioni 150 kama angesajiliwa mwisho wa usajili

“Usajili wa Lukaku na Matic sasa gharama yake jumla ingefika paundi milioni 200.Lakini kwa sababu tulisajili mapema tumetumia gharama ndogo sana. Nadhani tulifanya vyema katika upande wa kifedha na tulifanya maandalizi ya usajili vizuri”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents