Aisee DSTV!

Jose Mourinho ala za uso utabiri wa kombe la dunia

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amejikuta akiambulia patupu kwenye utabiri wake wa michuano ya kombe la dunia baada ya kuzitabiria timu ambazo zimeshindwa hata kutinga hatua ya nusu fainali.

Siku moja kabla ya kuanza kwa kombe la Dunia nchini Urusi kocha wa Manchester United, Jose Mourinho alizitabiria timu nne zitakazo pata nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa ambazo ni Ureno, Brazil, Argentina na Ujerumani.

Tazama utabiri wa Mourinho Hapa

Katika kuonekana Mourinho amekula za uso kwenye utabiri wake ni baada ya timu za Mataifa ya Ufaransa, Ubelgiji, Croatia na Uingereza kufika nusu fainali badala ya zile ambazo amezitabiria yeye hapo awali ambazo ni Ureno, Brazil, Argentina na Ujerumani.

Tayari mpaka sasa michuano hiyo imeshafikia hatua ya fainali ambapo Ufaransa itashuka dimbani kuikabili Croatia siku ya Jumapili.

Wakati mshindi wa tatu wa michuano hiyo akitarajiwa kupatikana siku ya Jumamosi wakati Uingereza itakapo wakabili Ubelgiji.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW