Burudani ya Michezo Live

Jose Mourinho azitabiria timu hizi kutinga nusu fainali kombe la Dunia nchini Urusi

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kuanza kwa kombe la Dunia hapo kesho nchini Urusi kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amezitabiria timu nne zitakazo pata nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa.

Kupitia mahojiano yake na chombo cha habari cha RT Sport, Mourinho amesema kuwa timu anazo amini kufika hatua hiyo ni Ureno, Brazil, Argentina na Ujerumani.


Michuano hiyo inayoanza hapo kesho siku ya Alhamisi itashuhudiwa mwenyeji Urusi akikabiliana na timu ya taifa ya Saudi Arabia kwenye mchezo wa ufunguzi huko Moscow.

Mourinho amekitabiria kikosi cha Uingereza kinachonolewa na kocha, Gareth Southgate kutinga hatua ya robo fainali na kuja kufungwa na Brazil itakayo pata nafasi hiyo ya kuingia hatua ya nusu fainali.

Huku akilitabiria taifa lake la Ureno kushinda dhidi ya Uruguay kisha kuju kuwafunga Ufaransa na kutinga hatua hiyo ya nusu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW