Michezo

Jose Mourinho kutimkia Bundesliga ?; ‘Kwa sasa najifunza Kijerumani’

Jose Mourinho afungua milango kwa klabu za Bundesliga baada ya kudai kuwa kwa sasa anajifunza lugha ya Kijerumani katika kipindi hiki ambacho hayupo kazini.

Image result for Jose Mourinho bundesliga

Mreno huyo ambaye ametumia muda wa miaka miwili na nusu kama kocha ndani ya klabu ya Manchester United kabla ya kutimuliwa mwezi Desemba baada ya kupokea kichapo mbele ya Liverpool katika dimba la Anfield.

Akiwa Manchester United, Mourinho amefanikiwa kuipatia timu hiyo kikombe cha League Cup, Community Shield na Europa League katika muda wake wa uongozi.

Licha ya kutimuliwa msimu wa mwaka 2017/18, Mourinho ametajwa kama kocha bora na aliyeipatia mafanikio makubwa. Mpaka sasa kocha huyo amehusishwa na kutakiwa klabu za Benfica, Lyon na Newcastle.

Kwa muda mrefu amekuwa akisema anasubiria mradi sahihi “right project”, hajawahi kufundisha timu yoyote ya Bundesliga, mpaka sasa amekuwa kocha katika baadhi ya klabu za Ureno, Itali, Hispania na Uingereza.

Alipoulizwa kuhusu mipango yake ya baadae, Mourinho ameiyambia Gazzetta dello Sport kuwa, “Hakia naumisi mpira. Nimemisi kuwa uwanjani, kazi yangu, mpira ni mpira.” – amesema Mourinho.

Mourinho ameongeza kuwa “Kwa sasa ninajifunza Kijerumani. Bundesliga kwa sasa ?, ninajifunza Kijerumani kwa sababu ninaimisi hii lugha. Ninazungumza Kiingereza, Kispania, Kireno, Kifaransa na Kiitalia lakini sifahu chochote kuhusu Kijerumani.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents