Michezo

Jose Mourinho kutua Tottenham, Manchester United kubadili gia angani sasa ni Mauricio Pochettino

Klabu ya Tottenham wamezidi kuonyesha nia ya kumtaka, Jose Mourinho huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu msimamo wa Manchester United wa juu ya kumpa mkataba, Mauricio Pochettino. (Daily Express)

Image result for jose mourinho

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86 kwa Mcolombia James Rodriguez mwenye umri wa miaka 28 anayecheza safu ya kati ili kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa N’Golo Kante. (El Desmarque, via Sport Witness.

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86 kwa Mcolombia James Rodriguez

Mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 33, anasakwa na Manchester United lakini ameonywa kuwa atahitaji kushusha kiwango cha madai yake ya mshahara. (ESPN)

Hata hivyo Manchester United wanahofu kuhusu ugumu wa kusaini mkataba mpya wowote na wachezaji wapya katika kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari . (Metro)Real Madrid wanamsaka N'Golo Kante

Real Madrid wanamsaka N’Golo Kante

Kocha wa Arsenal Unai Emery hatazamii kupanua kikosi chake mwezi Januari wakati wa kipindi cha uhamisho wa wachezaji. (The Athletic, via Mirror)

Mshambuliaji wa Chelsea Mfaransa Olivier Giroud,mwenye umri wa miaka 33, anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo mwezi wa Januari ikiwa hatacheza tena. Inter Milan na timu ya Ligi kuu ya Canada Vancouver Whitecaps ni miongoni mwa timu zinazomtaka. (Sun)Manchester United wanamtaka Mario Mandzukic ashushe viwango vya mshahara ili wamuajiriManchester United wanamtaka Mario Mandzukic ashushe viwango vya mshahara ili wamuajiri

Mchezaji wa safu ya kati wa Croatia Luka Modric amemuomba mchezaji mwenzake katika kikosi cha Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 30, akimtaka abakie katika klabu baada ya mshambuliaji huyo wa kati wa Wales kukaribia kabisa kuhamia Bernabeu msimu uliopita. (Independent)

Kiungo wa kati Mbrazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, bado anaweza kurudi Liverpool – ikiwa Bayern Munich wataaamua kutosaini mkataba wa kudumu na yeye msimu ujao . Kwa sasa anacheza kwa mkopo katika timu hiyo ya Ujerumani kutoka Barcelona. (AS, via TeamTalk)Olivier Giroud anajiandaa kutoka ChelseaOlivier Giroud anajiandaa kutoka Chelsea

Paul Ince, ambaye ni nahodha wa kwanza mweusi wa England, anasema angewaongoza wachezaji wenzake kuondoka nje ya uwanja kama angekuwa anacheza katika mchezo baina ya Bulgaria na England Jumatatu ambao ulitawaliwa na matusi ya ubaguzi wa rangi . (Times, subscription required)

Crystal Palace wanamtaka mshambuliaji wa safu ya kati wa Inter Milan Gabriel Barbosa, mwenye umri wa miaka 23, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Flamengo nchini Brazil. (PassionInter, via TeamTalk)Kocha wa Arsenal Unai Emery hatazamii kupanua kikosi chake

Kocha wa Arsenal Unai Emery hatazamii kupanua kikosi chake

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kuwaacha kiungo wa kati Muingereza Angel Gomes, mwenye umri wa miaka 19, winga wa Uholanzi Tahith Chong, mwenye umri wa miaka 19, na kiungo wa kati Muingereza James Garner mwenye umri wa umri wa 18, waondoke kwa mkopo mwezi Januari. (Mail)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents