Tupo Nawe

Joseph Kusaga akutana na Didier Drogba, amtangazia fursa na kuafikiana mambo makubwa

Mkurugenzi wa Kampuni ya Clouds Media Groups Ltd, Joseph Kusaga jana usiku amekutana na mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Didier Drogba nchini Marekani kwenye mchezo wa kikapu wa NBA ALL STARS 2019.

Joseph Kusaga na Didier Drogba

Kusaga ameeleza kuwa, baada ya kukutana naye wameongea masuala mengi ikiwemo uwekezaji kwenye michezo, ambapo Drogba ameridhia kuja Tanzania na kuwa sehemu ya uwekezaji.

Nimekutana na @didierdrogba – Didier Drogba. Drogba anaamini uwekezaji kupitia michezo unatakiwa na utasaidia sio kwenye kuwapa vijana nafasi bali pia kukuza uchumi wa mataifa husika. Akiwa tayari kuwa sehemu ya uwekezaji wa waliokuwa tayari, Nimemwambia Tanzania tutakuwa wa kwanza kumwita na ameridhia.,“ameandika Joseph kusaga kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW