Habari

Joseph Payne: Watanzania waone fahari kutumia lugha yao


Aliyekuwa mshindi wa pili kwenye shindano la Bongo Star Search mwaka 2010, muingereza Joseph Payne amewataka watanzania kuona fahari kuitumia lugha ya Kiswahili.
Akiongea kwenye kipindi cha ‘Lulu za Kiswahili’ cha TBC Taifa, Payne amesema watanzania wanapaswa kujivunia na lugha ya Kiswahili ambayo imeeneza zaidi Afrika kuliko lugha nyingine yenye asili ya barani Afrika.
Ameongeza kuwa anasikitishwa na kasumba iliyopo nchini ambapo kuna watu hudhani kuwa kujua kuzungumza Kiingereza ndio ustaarabu na usomi.
Payne ambaye huzungumza Kiswahili fasaha, amedai kuwa suala hilo ni la kupigwa na kwamba wananchi wanatakiwa wawe na msingi wa lugha yao kwanza kabla ya lugha za kigeni.
Muingereza huyo ambaye anafanya kazi kwenye ubalozi wa Uingereza nchini, amesema lugha ya Kiingereza iliweza kuenea dunia nzima kutokana na wananchi wake kuithamini lugha yao.
Mwaka 2010, Joseph Payne alijipatia umaarufu nchini kwa kuzikonga nyoyo za wapenzi wa BSS kutokana na uwezo wake wa kuimba nyimbo za Bongo Flava.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents