Michezo

Joshua kutetea ubingwa wake mbele ya muafrika

Bingwa wa dunia wa uzito wa juu, Anthony Joshua atakuwa na kibarua kizito cha kutetea ubingwa wake wa IBF na WBA pale atakapo vaana na bondia, Carlos Takam mzaliwa wa Cameroon Octoba 28 mwaka huu.

Hapo awali Joshua alipangiwa kupigana na Kubrat PulevĀ  katika uwanja wa Cardiff lakini bondia huyo ameamua kujitoa kufuatia majeraha aliyopata katika bega wakati akijiandaa na mchezo huo.

Anthony Joshua mwenye umri wa miaka 28 ataingia ulingoni kwa mara ya kwanza tangu alipopata ubingwa mbele ya Wladimir Klitschko katika dimba la Wembley April.

Joshua atapambana na Takam ambaye anaishi nchini Ufaransa huku mpaka sasa jumla ya tiketi 70,000 zimeshauzwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents