Burudani

Joti aja kivingine ni msimu wa pili wa tamthilia ya vichekesho ya Mwantumu,kuonyeshwa na DStv mwanzo mwisho (+Video)

Kuonyeshwa kupitia Maisha Magic Bongo chanel nambari 160 mara mbili kwa wiki

Msimu mpya wa vichekesho maarufu vya Mwantumu ambavyo huonekana kupitia chaneli ya DStv ya maisha Magic Bongo unaanza rasmi jumanne ya octoba 16,huku vikiwa vimeongezewa manjonjo ili kuwa hakikishia watazamaji na mashabiki wake burudani isiyo na upinzani.

Vichekesho hivyo vinavyoongozwa na mchekeshaji maarufu nchini Lucas Mhuvile maarufu kwa jina la kisanii Joti ambaye ambaye kwenye vichekesho hivyo amevaa uhusika wa watu watatu tofauti; Mzee Mrisho, Kaboba na Mwantumu Sahare, vimekuwa ni moja ya vipindi vinavyotazamwa sana na kupendwa na maelfu ya watu hapa nchini ambavyo huonyeshwa kupitia chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo DStv chaneli namba 160.

Majina maarufu pia katika tasnia ya uigizaji na uchekeshaji yatakuwepo msimu huu akiwemo mzee Fungafunga ,Mzee mwalubadu,Mama Abduli ,Mwantumu Mcharuko,Alex Wasponga (Kayombo) na Wengine wengi.\

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa vichekesho hivyo,mkuu wa masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema kuwa tangu kuanza kwa msimu wa kwanza wa vichekesho vya Mwantumu mnamo octoba 207, vichekesho hivyo vimekuwa na msisimko wa aina yake na vimepokelewa vizuri sana na watazamaji na hivyo kuvifanya kuwa na mashabiki wengi sana.

Katika msimu huu mpya vichekesho hivyo vitaonekana mara mbili kwa wiki siku ya Jumanne na Jumatano saa moja na nusu usiku.hii itawapa fursa mashabiki na watazamaji wa Maisha Magic Bongo kupata burudani zaidi kwani kumekuwa na maombi mengi ya kuongeza vipindi hivyo kutokana na umaarufu wake alisema Alpha.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents