Michezo

Joti atoa ya moyoni kuhusu matokeo ya Taifa ” Hao Cape Verde walituonea huruma kutufunga hizo goli tatu” (+Video)

Awacharukia wanaowaponda akina Samatta na Ulimwengu

Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Lucas Mhuvile alimaarufu Joti amefunguka na kutoa ya moyoni kuhusiana na matokea ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kupoteza ugenini nchini Cape Verde kwa kufungwa jumla ya goli tatu kwa sifuri.

Joti amesema hayo wakati anapiga stori na Bongo five siku ya uzinduzi wa tamthili yake ya Mwantumu ambayo imerudi kivingine katika msimu wa pili ambayo itakuwa inaruka kupitia Chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo kila siku za Jumanne na Jumatano saa moja na nusu usiku.

“Cape Verde kutufunga hizo goli tatu walituonea huruma sana kwani inawachezaji wakubwa sana wanaochezea nje sio ukumu letu kuanza kujilaumu,timu inapopangwa tuwe tunatoa maoni mapema””Halafu TFF wafanye mpango watu waingie bure uwanjani,kwani washabiki wanachoka na wachezaji wanachoka kusemwa ila mtu ukiwa kwako inatia hamasa sana”

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents