Michezo

Joto la Ilala ‘Derby’ Simba v Yanga lapanda

Joto limezidi kuongezeka kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu kongwe nchini za Yanga na Simba kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kupigwa tarehe 23 ya mwezi huu katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Vikosi vya Simba na Yanga vikiwa vipo Uwanjani tayari kwa Mchezo

Nchi itakuwa kimya kwa dakika 90 kupisha Darby hii inayoshika namba tatu kwa ukubwa Afrika baada ya kwanza ikiwa ni ile ya Al Ahaly vs Zamalek ya pili Kaiser Chiefs vs Orlando Pirates  wakati ya nne ni Gor Mahia dhidi ya AFC Leopard  ambapo zinapo kutana kila haina ya vituko hujitokeza uwanjani.

USAJILI: Simba SC yango’a kiungo hatari wa Azam dakika za majeruhi

USAJILI: Simba SC sasa hizi kufuru yampa mkataba Golikipa Bora COSAFA

Ukubwa na uzito wa mchezo wa Yanga SC  na Simba SC ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa unachagizwa hasa kutokana na ukongwe wa timu hizi hasimu zinazopishana mwaka mmoja katika kuanzishwa kwake wakati watoto wa Jangwani ikiwa 1935 huku hasimu wake wekundu wa msimbazi akizaliwa 1936 ambapo wote hawa wanapatikana katika wilaya moja ya Ilala.

 

Mashabiki wa klabu ya Simba wakishangilia timu yao bila kukata tamaa

Usajili uliyofanywa na klabu hizi unafanya kuongeza joto katika mchezo huo hasa kutokana na majina na haina ya wachezaji waliyosajiliwa kwa msimu huu.

Mashabiki wa klabu ya Yanga wakiwa wapo pamoja na timu yao mpaka mwisho wa mchezo bila kuchoka

USAJILI: Yanga SC yapata mbadala wa Msuva

USAJILI: Yanga SC yamalizana na Kamusoko

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hapo jana limetoa taarifa juu mchezo huu ambao matokeo yake hutengeneza historia kwa timu zote mbili.

Maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaowakutanisha Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/17, Young Africans na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup), Simba yanakwenda vema.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwatangazia umma kuwa viingilio katika mchezo huo vimepangwa katika makundi manne.

Sehemu ya VIP ‘A’ tiketi zake ni Sh 25,000; sehemu ya VIP ‘B’ na ‘C’ Sh 20,000; Viti vya Rangi la Chungwa Sh 10,000 na mzunguko kwa vitu vya rangi za bluu na kijani ni Sh 7,000.

Tiketi zimeanza kuuzwa leo Jumanne Agosti 15, 2017 ili kuwapa fursa wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi mapema kujipeusha na usumbufu.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents