Uncategorized

JS Saoura FC waanza kuwachunguza Simba, wahofia wingi wa mashabiki Taifa, CAF Champions League

Wapinzani wa Simba kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika, klabu ya JS Saoura inayoshiriki ligi kuu ya Algeria maarufu kama League Professionelle 1 imeonekana kama kuanza kuwachunguza wawakilishi wa Tanzania Wekundu wa Msimbazi kabla ya kuwakabili tarehe 11/1/2019.

Kupitia mtandao wao wa kijamii wa Facebook miamba hiyo ya soka ya Algeria, JSsaoura imeanza kuposti baadhi ya matukio yanayowahusu Simba SC inayo waonyesha kuwafatilia kwa ukaribu, uwezo wa wachezaji  na hata wingi wa mashabiki wake kwenye michezo ya Kimataifa.

This image has an empty alt attribute; its file name is Duuuu-600x301.jpg

Desemba 30 siku ya Jumapili JSsaoura FC kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook iliposti picha ya kikosi cha Simba ambacho kilicheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida United huku wakiandika ujumbe kuwa  habari za mpinzani wetu leo amepata matokeo ya ushindi.

“Habari za mpinzani wetu, leo mpinzani  wetu Simba amepata matokeo ya ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Singida United katika mechi ya ligi kuu ,’’ wameandika JSsaoura.

JS saoura FC pia waliposti kipande cha video kinachowaonyesha mashabiki wa Simba walivyo furika kwa wingi kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Nkana FC ya Zambia.

“Hivi unajua ndugu yangu wa Soura, hizo ni kelele zamashabiki wa Simba katika uwanja wao wa Taifa uliyopo kwenye mji wao mkuu wa Tanzania mchezo wao mwisho dhidi ya Nkana,’’ wameandika.

Klabu hiyo ya Algeria imeongeza ‘’Kiukweli  tuliwahi kuona mechi nyingi kwenye uwanja huu dhidi ya Tanzania kukiwa na mashabiki wachache lakini mashabiki hawa wamezidi, uwanja umefurika. Rabbi (Mungu) Tujibu yaliokuwa ya Kheri.’’

Hivi ndivyo JSsaoura FC wanavyoendelea kukusanya taarifa za mpinzani wake Simba ili kuweza kumjua udhaifu wake na pengine kuwa rahisi kupata matokeo kwenye mchezo wao ujao na wameanza kufanya hivi baada ya kujua wamepangwa kundi moja na miamba hiyo ya soka ya Tanzania.

Hii si mara ya kwanza  kwa klabu ya JSsaoura kufanya hivyo, wamefanya hata kwa mabingwa wa Morroco IR Tanger na wamefanikiwa kuwatoa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani na kufungwa 1-0 ugenini. Hata hivyo wameonyesha hofu yao kwa wingi wa mashabiki waliyonao Simba.

Timu hizi hazijawahi kukutana kwenye michuano yoyote na hivyo hiyo itakuwa mara yao ya kwanza kukutana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents