Burudani

Juacali amfagilia Rayvanny

By  | 

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Kenya, Juacali ameonyesha kfurahishwa na msanii Rayvanny.

Akiongea na mtangazaji wa Citizen Radio ya Kenya, Mzazi Willy Tuva katika kipindi cha Msetoea, rapper huyo amemsifia msani huyo kutoka WCB, kwa kusema ushindi wake unaupa sifa muziki wa East Afrika kwa kuutangaza zaidi.

“Unajua dream yetu sisi wote ni kupeleka ngoma za East Afrika huko nje. Unajua competition ziko nyingi sana, tunapigana na watu wa South Africa, West Africa, Marekani, watu wa Europe and the moment kuna msanii wetu anashiunda tuzo kama hiyo, kwa sababu hiko ni kitu kikubwa sasa kinaweka East Afrika mahali pazuri especially kwanza kiswahili. Unajua mimi ni mtu wa wa Kiswahili so nikiona msanii anaimba kwa Kiswahili na ameshinda inapendeza sana.”

Juacali ameahidi kuachia albamu yake ya nne mwezi Septemba mwaka huu ambayo ameipa jina la ‘Mali ya Umma’.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments