Habari

Julius Mtatiro ang’atuka CUF  ‘hitaji la nafsi yangu ni kujiunga na CCM’

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ametangaza kuachana na chama hicho hii leo Agosti 11 na kuonyesha nia ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mtatiro ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari hii leo huku akitaja maeneo matano ambayo yamemfanya kujiengua na CUF na kuamua kuunga mkono juudi za Rais John Magufuli.

”Nilichoomba kukutana na nyinyi ni kutangaza mustakabali wangu katika siasa za nchi yetu. Ninauchambuzi binafsi katika maeneo mbalimbali ambayo mimi ninashiriki kama mwanasiasa, kama kijana na kama kiongozi,” amesema Julius Mtatiro aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF.

Mtatiro ameongeza ”Katika tafakari yangu hiyo nilipitia maeneo kama matano ambayo nimeyafanyia kazi. Eneo la kwanza niliangalia ushiriki na mchango wangu kwenyesiasa za chama cha wananchi CUF, eneo la pili ilikuwa ni mgogoro unaoendelea kukikumba chama cha wananchi CUF, eneo la tatu ambalo nimelitafakari kwaupana sana ni ushiriki wangu kama kijana na kama kiongozi katika kuchochea maendeleo ya nchi, eneo la nne lilikuwa ni ajenda muhimu za usimamizi na uendeshaji wanchi na eneo la mwisho kwamaana la tano ilikuwa nimustakabali wangu kisiasa,” amesema Mtatiro

”Hayo ni maeneo matano ambayo nilijipima mwezi mzima kuyapekuwa kwa kadri ambavyo nimeweza, kwahiyo nimejipa huo muda wakutosha lakini pia nimewahusisha marafiki zangu, washauri wangu wakubwa, nimewahusisha ndugu zangu, familia yangu lakini pia nimezingatia kwamba unapokuwa kiongozi na mshiriki wa siasa zanndani ya nchi yako lazima kilawakati ujikague na kuamua hatma nje kuhusu ushiriki wako.”

”Lakini pia nimezingatia kwamba unapokuwa kiongozi na mshiriki wa siasa zanndani ya nchi yako lazima kilawakati ujikague na kuamua hatma nje kuhusu ushiriki wako. Nilikuwa CUF kwasababu nilikuwa nahitaji kushiriki kutatua shida na matatizo ya Watanzania, kwasababu nimeona nikiwa CUF ulingo wakutimiza hadhima hiyo nifinyu nimeamua sasa kujiunga na chama cha Mapinduzi nakama nilivyoeleza uwamuzi huo nitautekeleza mara moja baada ya kuwasiliana na kukubaliwa na viongozi wachama hicho.

Mtatiro amesema kuwa anahitaji kufanya siasa za kuleta maendeleo ya nchi yake na amejiridhisha kwamba huu ni wakati muafaka wa kuwatumikia Watanzania.

Related Articles

4 Comments

  1. …ninaona vyeo vifuatavyo vinakuhusu kwa kuwa zile nafasi za upendelea za UBUNGE zimeisha. Nazo ni: Ukuu wa Mkoa yaani RC, RAS, DAS, Ukurugenzi wa Halmashauri, uenyekiti wa bodi mojawapo ya shirika au taasisi fulani au hata ujumbe kwenye TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI ili uzichange karata vizuri. Hakika naona wanasiasa wa zama hizi ‘nyoyo’ nyepesi mno kuliko hata ’tissue papers’ aisee. Yaani wewe Julius Mtatiro kwa ile misimamo madhubuti ya miaka na ‘mikaka’ ndio ‘umelainika’ namna hii? Au majuzi hapa ‘walipokushikilia’ na hata kuchukua mawasiliano yako kwa maana ya simu ndipo umeamua ‘ku-surrender’ kienyeji namna hii?! Kweli njia ya kuelekea ‘peponi’ kwa mwanadamu ni ‘nyembamba’ mno!

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents