Burudani ya Michezo Live

Juma Kaseja na mkewe wapata watoto mapacha

Mlinda Mlango wa Klabu ya Mbeya City, Juma Kaseja na mke wake wamepata watoto mapacha.

12144039_1619629391634776_1705202940_n

Taarifa hiyo imetolewa na Idris Sultan aliyempongeza mchezaji huyo kwenye Instagram.

“Napenda kutoa pongezi zangu taaaaaaaaaaaaaaamuuuuu ziwaendee @official_juma_kaseja na Mkewe Nasra kwa kupata twins jana wa kiume na wa kike,” ameandika Idris.

“Alhamdullillah mwenyezi kawaleta wazima na wazazi wote wazima nikimaanisha Nasra yupo feeshi kabisa na Juma hajazimia. Wa kiume nadhani wanapanga kumuita Idris. Allah awazidishie baraka. Sasa juma ndoto za kuota unapiga danadana acha bro Nasra kanilalamikia sana hata jana wakati nahudumia wagonjwa akanipigia nimpe moyo kua hautamshuti mtoto mmoja kama mechi ya juzi ila tuachane nayo hayo nipo shopping nanunua vitunguu jana viliisha, nanunua na karoti jamani tumpongezeni Juma sio mcheza mpira tu ila mechi zote.”

Naye Kaseja alijibu kwa kuandika: Asante sana mungu mkubwa na ndio mpangaji wa kila jambo asante mungu kwa kunipa wawili asnte IDRIS.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW