Burudani

Juma Nature: Dini lenye thamani lililokosa muuzaji

Mwenyezi Mungu ametupa vipawa mbalimbali na jinsi ya tofauti kabisa. Pengine ndio sababu unaweza ukafanya kila kitu ambacho fulani anafanya na usipate matokeo kama yale anayoyapata huyo mtu. Sijui kwanini, lakini pengine ndiyo sababu Mungu akaitwa Mungu.

Unamjua msanii ambaye anapendwa zaidi na mashabiki? Unamjua msanii ambaye uwepo wake kwenye show unamaanisha wasanii wengine inabidi wagombanie nafasi ya pili kwani nafasi ya kwanza ni yake? Unamjua msanii ambaye hata asipotoa hit miaka mitano ila akipanda jukwaani lazima aache jukwaa linazizima? Jibu lako lisipokuwa Juma Nature utakuwa pengine umeanza kuufuatilia muziki wa Bongo jana.

Ndiyo,Juma Nature Kiroboto anapendwa na ana nguvu ya pekee na ya tofauti kabisa. Mashabiki wanampenda mjamaa Juma Kassim tena pengine bila hata sababu za msingi. Ni miongoni mwa watu wachache ambao Mungu aliwajalia mvuto wa kipekee ambao pengine sio juhudi wala maarifa yoyote yanaweza kukufanya upate kile alichonacho.

Lakini kuna kitu kinachonishangaza, hivi Juma Nature yeye mwenyewe hajui ni jinsi gani alivyo dini adhimu kwenye muziki wa nyumbani? Hivi ni kweli makampuni, wadau na mameneja hawaoni kuwa Juma ni bidhaa ambayo wateja wanasubiri muda wowote waambiwe wapi inapatikana waende wakainunue hata kama kwa gharama kubwa?

Moja kati ya kazi kubwa katika marketing ni kuintroduce bidhaa kwa watu,lakini kama bidhaa tayari inahitajika ni kazi rahisi kuiuza hiyo bidhaa. Juma Nature wala haitaji kutambulishwa,pengine ni yeye au mtu kumsaidia kuwa brand. Watu wanaofanya biashara ya muziki ni kuwa hawajui hili au kuna tatizo kwa Juma Nature kukubali kufanya biashara na watu?

Kuna tatizo kubwa katika ishu ya branding kwenye nchi yetu,wasanii na wadau pamoja Na watu wanaowazunguka hawajui kutumia nguvu waliyonayo kwenye jamii. Juma Nature ni mkubwa sana kwa jinsi Mungu alivyompa karama ya aina yake hatakiwi kuwa alivyo,wafanyabiashara ya muziki hakuna bidhaa adimu kwenye muziki kama Juma.

By Eliezer Gibson aka greencitynative
IG:gibson_elly
0769346186

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents