Michezo

Jurgen Klopp apelekwa hospitali

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amekosekana uwanjani hii leo wakati kikosi chake kikiwa katika mazoezi baada ya kutojiskia vizuri kiafya na hivyo kwenda hospitali.

Klopp amefanyiwa uchunguzi wa afya yake na madaktari wa timu hiyo na kuruhusiwa jioni.

Kikosi kizima cha Liverpool kilirejea Melwood baada kukosekana kwa kocha Klopp.

“Amefanyiwa uchunguzi wa afya na madaktari, amekosekana katika mazoezi ya Jumatano,” maelezo kutoka ndani ya klabu ya Liverpool.

“Hakuna mpango wa Jurgen kubaki hospitali makubalino ni kwamba atarejea nyumbani kwake jioni hii.”

Miongoni mwa wachezaji waliyorejea katika mazoezi baada ya kutoka kuzitumikia timu zao za taifa ni Philippe Coutinho, Roberto Firmino, Simon Mignolet, the Reds inajianda kuikabili Southampton siku ya Jumamosi.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents