Michezo

Jurgen Klopp avunja rekodi Uingereza

Klabu ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imeonekana kuwa ndiyo timu yenye kupata matokeo bora zaidi dhidi ya zile zilizopo ndani ya sita bora ya Epl tangu inolewe na Meneja, Jurgen Klopp.

Liverpool imekuwa yenye mafanikio makubwa miongoni mwa timu kubwa za Uingereza tangu, Jurgen Klopp kurithi mikoba ya Brendan Rodgers katika dimba la Anfield mwezi Octoba mwaka 2015.

Chini ya Klopp, Liverpool imeshinda michezo yake ya ligi kwa asilimia 47 huku ikivuna alama 33 katika michezo yake 18 iliyokutana na miamba ya soka ya Uingereza Tottenham, Manchester City, Arsenal huku ikishindwa kufanya hivyo mbele ya Manchester United mwezi Januari mwaka uliyopita.

 

Kwa ushindi wao wa michezo tisa ikijumuisha mitatu dhidi ya Manchester City,mitatu na Arsenal miwili mbele ya Chelsea na mmoja dhidi ya Tottenham.

Huku Arsenal ikipokea kipigo cha mabao 4-0 chini ya Meneja Klopp mchezo uliyopigwa katika dimba la Anfield mwezi uliyopita.

Je Liverpool itaendeleza rekodi yake mbele ya Manchester City katika dimba la Etihad siku ya Jumamosi ?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents