DStv Inogilee!

Justin Bieber afikiria kufanya show za bure kama surprise kwa mashabiki


Akiwa na utajiri wake mwenyewe unaofikia dola milioni 105 na zaidi, Justin Bieber mwenye miaka 18 tu, anaweza kuamua lolote!

Hebu fikiria kuanzia May 2010 hadi May 2011 dogo aliingiza dola milioni 53. Kwa umri wake anashindwa nini kuamua kufanya tu show za bure ili kuwafurahisha mashabiki wake?

Kila show moja unayosikia amefanya sehemu si chini ya $600,000 inakuwa imeshawekwa kwenye akaunti yake.

Ndio maana katika kuonesha kuwa hela si kitu kwake tena jana usiku ametweet, “am i about to be doing free shows around the world to surprise fans?? hmmm. #staytuned #BELIEVE.”

Mashabiki wake wana haki ya kuamini maneno yake kwakuwa mafanikio aliyoyapata katika umri huo mdogo hayawezi kuathiriwa kwa uamuzi wake wa kupiga show mbili tatu za bure ili kuwasurprise mashabiki wake.

Ingependeza ofa hiyo akaitoa kwa nchi kama Tanzania ambayo promoter akimleta kuperform show moja kwa dola laki sita ni ngumu hata kurudisha mtaji achilia mbali kula za uso!

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW