Burudani

Justin Bieber ni miongoni mwa mastaa waliosign kwenda safari ya utalii wa angani ‘Outer Space’

Imefahamika kuwa msanii mdogo anaeandikwa sana mtandaoni kwa sasa Justin Bieber ame sign kwaajili ya safari ya utalii wa angani mapema mwakani ‘outer space’.

justin-bieber-outerspace-lead

Pop Sensation Justin Bieber mwenye miaka 19 na meneja wake Scooter Braun wamesign na kampuni ya Virgin Galactic , inayotoa huduma ya ‘space flights’ kwaajili ya safari ya utalii wa angani ‘space tourism’.

Taarifa hiyo ilipatikana (June 5) kutoka kwa muanzilishi wa Virgin bwana Richard Branson aliyetweet akitoa taarifa juu ya Bieber na meneja wake kuongezeka katika orodha ya zaidi ya watu 500 watakaoenda safari ijayo, “Great to hear @justinbieber & @scooterbraun are latest @virgingalactic future astronauts,” tweeted Branson. “Congrats, see you up there!” , tweet ambayo Bieber alii re-tweet.

Pamoja na Bieber, mastaa wengine ambao watakuwa katika safari hiyo ni pamoja na Ashton Kutcher, Brad Pitt na Angelina Jolie.
Inagharimu kiasi cha $250,000 sawa na zaidi ya million 400 za Tanzania kuweza kuwa miongoni mwa wasafiri wa kwenda trip hiyo ya utalii wa angani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents