Michezo

‘Juuko Murshid ametoroka, tulisikia yupo Abu Dhabi, atakula adhabu wala hataenda kokote,’ – Mtendaji Mkuu Simba  Crescentius Magori (+video)

Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Crescentius Magori amesema kuwa beki wao wa Kimataifa wa Uganda, Juuko Murshid ametoroka licha ya kuwa na mkataba huku akitoa kisingizio cha kuumwa wakati akionekana na timu yake ya taifa Wakifanya mazoezi.

Mkurugenzi huyo, Magori ameyasema hayo hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena.

”Juuko Murshid anamkataba na Simba mpaka mwisho wa msimu, wakati timu imeenda kucheza Kanda ya Ziwa amesema anaumwa akabaki Dar Es Salaam kujiuguza majeraha.”

Crescentius Magori ameongeza kuwa awali alisema anaumwa na kubaki Dar Es Salaam kisha kutimkia kwao Uganda.

”Timu ilivyokuja Dar Es Salaam akawa tayari ameshatoroka amekwenda Uganda, hakumuaga kocha, meneja hakuaga uongozi.”

”Wakati akidai hawezi kufanya mazoezi tukasikia yupo Abu Dhabi na timu ya taifa ya Uganda anafanya mazoezi kule, tukamuandikia barua ajieleze ni kwa ni kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu, kwa kuondoka kituo chake cha kazi bila ruksa ya muajiri, hata kuongea na kocha wala meneja hiyo barua hakuijibu mpaka leo.”

”Juzi timu ilipoanza kazi tulimuandikia aripoti kituo chake cha kazi, kabla ya tarehe 15, hajaweza kuripoti.”

”Juuko anafikiri kwamba anaweza kulazimisha kuhama, hawezi kulazimisha kuhama na kwasababu ametoroka kazini mshahara wa mwezi wa tano hatukumlipa na wa mwezi wa sita pia tutamlipaje mtu ambaye hayupo kazini.”

”Tumemuita Dar Es Salaam ili tuweze kuzungumza, tunamshitaki kwenye kamati ya nidhamu ili atowe majibu yake, kwa nini alitoroka kambini bila ruksa.”

”Hatua ambazo tutachukua ni ya upande mmoja kwasababu hataki kufikia katika kituo chake cha kazi huku akiwa na mkataba, kanuni za FIFA zinatulinda, sekta zote zinatulinda na ukiwa na mkataba hata ufanyaje huwezi kuondoka.”

”Kama ana timu amepata ije ili izungumze na Simba, lakini kama anazunguka zunguka tu basi atakula adhabu wala hataenda kokote mpaka mkataba wake utakapoisha mwezi Desemba.”

Mara kadhaa beki huyo amekuwa akihusishwa na tabia ya utoro huku klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusinilakini iliwahi kuhusishwa kumnyemela nyota huyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents