Michezo

Juve yakumbushia yaliotokea mwaka 1996 Old Trafford

Kwamara ya kwanza klabu ya Juventus inafanikiwa kupata ushindi kwenye uwanja wa Old Trafford michuano ya Champions League tangu ilivyowahi kufanya hivyo mwezi Novemba mwaka 1996, walipoibuka na bao 1-0 chini ya alieykuwa kocha wao Marcello Lippi.

Manchester United hapo jana imejikuta ikipoteza mchezo huo mbele ya Juventus kwa bao 1 – 0 lililofungwa dakika ya 17 ya mchezo huo.

Katika mchezo huo aliyekuwa nyota wa United, Ronaldo amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake ya Juve kuibuka na ushindi ambapo Paulo Dybala hakufanya ajizi na kujiandikia bao lake la tano msimu huu.

Wachambuzi wa soka wanasema kuwa Manchester United imeshindwa kuwa na matokeo mazuri kwenye uwanja wake wa nyumbani michuano hii ya Champions League tangu mwezi Novemba mwaka 2005.

Kikosi cha Manchester UnitedDe Gea (9), Young (7), Lindelof (7), Smalling (5), Shaw (5), Matic (6), Mata (4), Pogba (5), Rashford (4), Lukaku (3), Martial (4).

Mchezaji wa akiba, None

JuventusSzczesny (6), Cancelo (8), Bonucci (7), Chiellini (7), Alex Sandro (8), Matuidi (6), Bentancur (8), Pjanic (6), Dybala (8), Cuadrado (6), Ronaldo (7).

Wachezaji wa akibaBarzagli (6), Costa (N/A), Berardeschi (6)

Mchezaji bora wa mechi hiyo, Paulo Dybala.

Mpaka sasa ni Lionel Messi na Edin Dzeko ndiyo wanao ongoza baada ya kufunga magoli (5) kila mmoja michuano hii ya Champions League huku nyota huyo wa Juventus, Paulo Dybala akiwa amefunga magoli (4).

Matokeo ya michezo mingine nikama unavyoona hapo chini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents