Burudani

Jux adai hawezi kufanya show za kampeni za kisiasa

Mwimbaji wa muziki wa R&B, Jux amesema hawezi kufanya show za kampeni za kisiasa kwa kuogopa kuwachanganya mashabiki wake.

3b4c0a35c503b6623a260af30d902861

Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Jux alisema akipanda kwenye majukwaa ya siasa itakuwa ni kama anawashinikiza mashabiki wake kuchagua viongozi wasiowataka.

“Watanzania tulivyo, mimi kama kuna mtu ananipenda mpaka akaamua kuchora Jux au akaandika Jux kwenye mwili wake, mtu huyo nina nguvu ya kumshawishi na akafanya kitu bila ya yeye kutaka,” alisema.

“Kwahiyo leo nikisimama kwenye stage nikasema tumchague mtu fulani, kuna watu wengi sana katika akili zao watasema hata Jux mwenyewe kamchagua mtu fulani. Ndio maana hata viongozi wa siasa kwenye kampeni zao wanachagua wasanii ili kushawishi. Kwahiyo mimi naomba kama shabiki wangu uniangalia, mimi mwenyewe ni siri yangu, kuna kiongozi ambaye namuamini. Lakini wewe angalia mwenyewe, nenda Chadema au CCM. Msikilize Magufuli au Lowassa, wewe si una akili?”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents