Burudani

JUX aeleza chanzo cha kutumia jina mbadala la ‘African Boy’ hadi kuwa brand ya mavazi

Kama ulikuwa bado hujui kwa nini msanii wa muziki wa Bongo Fleva, JUX anatumia sana jina la ‘African Boy’ ukweli ni kwamba jina hilo limetokea huko nchini China kipindi anasoma.

JUX

JUX amesema kipindi anasoma nchini China wanafunzi wengi wenye asili ya China walikuwa hawaamini kama yeye anatoka Afrika kutokana na Swaggz na muonekano wake wengi walikuwa wanajua anatoka Marekani.

Ameleza kuwa huo ndio ulikuwa mwanzo wake wa kuanza kutumia Hashtag ya #AfricanBoy kwenye mitandao ya kijamii kama utambulisho kuwa anatoka Africa kwenye kila Posti aliyokuwa anaweka.

Miaka mingi iliyopita wakati nasoma China watu wengi niliyokuwa nakutana nao wenye asili ya China walikuwa wananiuliza unatoka wapi? nikawa nawambia natoka Afrika lakini walikuwa hawaamini kutokana na mavazi yangu, Cheni shingoni, suti kali walikuwa wanasema natoka Marekani, nadhani walikuwa wanaamini watu wengi wa Afrika hawawezi kuvaa vizuri wakapendeza walikuwa wanajua ni watu bado wanavaa majani, hivyo, nilikuwa nachukia sana na ndio nikaanza kutumia hashtag ya African Boy kwenye posti zangu za Instagram kama utambulisho wangu wa kiafrika,“amesema Jux kwenye mahojiano yake na kituo cha Runinga cha K24 cha nchini Kenya.

Baadaye baada ya kuona Hashtag hiyo imekuwa utambulisho wake mkubwa mitandaoni akaamua aitengeneze kuwa Brand na kuitumia kutengenezea bidhaa kama Nguo, Kofia, Fulana, Viatu na Cover za simu.

Na ndio nikapata wazo la kutengeza Logo ya African Boy ile logo inamuonesha mmasai amevaa cheni ya dhahabu na nikaanza kuona watu wanapendezwa zaidi na jinsi ninavyovaa na ndio nikaitengeneza rasmi African Boy kuwa Brand ya mavazi nakumbuka nilianza na kofia 50 na siku nimeleta ndani ya masaa mawili niliuza kofia zote na mpaka sasa ni brand kubwa natengeneza Kofia, Fulana, Viatu, Tracksuit na bidhaa nyingine,“amesema Jux.

Jux ambaye yupo nchini Kenya alikomsindikiza Vanessa Mdee kwa ajili ya uzinduzi wa album yake Money Mondays na akiwa huko ameahidi mwaka huu kufungua tawi la maduka yake ambapo bidhaa zote za African Boy zitapatikana.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents