Burudani

Jux asema wimbo wake mpya ‘Nitasubiri’ anaotarajia kuutoa hajamuimbia Jackie Cliff

Mwimbaji wa R & B Jux anatarajia kuachia wimbo mpya wiki hii uitwao ‘Nitasubiri’ ambao wengi wameuunganisha na tukio la kukamatwa kwa mrembo Jackie Cliff nchini China hivi karibuni, ambaye amekuwa akisemekana kuwa ni mpenzi wake.

jux 2

Akizungumzia wimbo huo, Jux amekiri kwamba ni kweli ameuandika baada ya Jackie kukamatwa China, na pia amekubali kwamba umebeba stori ya mtu anayemuimbia mpenzi wake ambaye ameondoka na kumuacha, au yuko safari kitu kinacholeta connection kubwa na Jacky hasa kwa kipindi hiki.

jux na Jackie
Jux na Jackie Cliff

“Nitasubiri ni wimbo ambao ni kweli ni nyimbo ya mapenzi” alisema Jux,” inaelezea kwamba kusubiri kwa mapenzi kuna aina nyingi unajua, kuna safari, kuna wewe kuondoka kumuacha mpenzi wako, mi nimejaribu kufanya utofauti tu kwasababu nimeimba nyimbo nyingi sana.”

Jux aliendelea kuuelezea wimbo huo,

“Nimeshamwimbia dem nampenda, nimeshamwimbia dem namsifia, nimeshamwimbia dem nagombana naye, kwahiyo kuna utofauti flani mapenzi yana vitu vingi. Sema labda kutokana na ile ishu ilivyotokea na watu wanavyoona si unajua kujumlisha kwahiyo ikaonekana kitu flani.” Jux aliiambia E News ya EATV.

jux nitasubiri

“Halafu na feelings tu nilizipata, mi nafanyaga muziki sababu nina feelings, hii nyimbo nimefanya kipindi hiki wakati nimerudi na hayo mambo yalikuwa yameshatokea, kuna mambo mambo yametokea maskendo ivi na ivi na ivi, kwahiyo niliingia tu studio nikaskiliza beat hisia zangu zikanijia nikaandika nyimbo ambayo iko vile.”

Jux ameendelea kukana kutokuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na Jackie zaidi ya urafiki, na kuongeza kuwa kwasasa ana mpenzi mwingine lakini hakuwa tayari kumtaja jina.

Wimbo mpya wa Jux ‘Nitasubiri’ unatarajiwa kutoka kesho Jumanne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents