Habari

JWTZ lakiri kudaiwa bilioni 3 na Tanesco, kuanza kupunguza deni hilo leo

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekiri kudaiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Shilingi bilioni 3 na kwamba linatarajia kuanza kupunguza kiasi cha deni hilo kwa kwa kuanza kulipa Shilingi bilioni moja leo.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akiongea na wanahabari Jumapili hii ambaye alibainisha wazi kuwa tayari Tanesco wamelipatia jeshi notisi ya kukatiwa umeme katika vituo vyake vyote leo, endapo deni hilo lisipolipwa.

“Hivi karibuni tumepokea taarifa ya Tanesco kuhusu kusitisha huduma kwenye vituo vyetu vyote kesho (leo) kutokana na deni kubwa tunalodaiwa. Hii ni kutokana na agizo la Rais John Magufuli kwa shirika hilo, kuwa liwakatie huduma wale wote wanadaiwa na shirika hilo, tunadaiwa kiasi kinachozidi kidogo bilioni 3 na Tanesco peke yake ” alifafanua Jenerali Mabeyo.

“Tayari nimeagiza watendaji wetu watafute kiasi cha Shilingi bilioni moja ili kesho (leo) hundi ipelekwe haraka Tanesco kwa ajili ya malipo, na kuzuia tusikatiwe umeme,” alieleza.

Aidha Mabeyo alibainisha kuwa pamoja na deni hilo la Tanesco, pia JWTZ inadaiwa na wazabuni wengine wanaotoa huduma kwao na tayari Hazina imeanza kulipatia jeshi hilo fedha kidogo kidogo ili kupunguza madeni hayo tuna imani tutayamaliza katika muda mfupi ujao kwasababu tayari serikali imeanza kutekeleza hilo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents