Habari

K-Lynn azungumzia maisha yake kama mama, kwanini hawezi kurudi kwenye muziki na kazi ya interior design (Video)

Ni nadra sana kukutana na Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi maarufu kama K-Lynn lakini kupitia tuzo za watu tulifanikiwa kupiga story mbili tatu.

K-Lynn ameiambia Bongo5 kuwa maisha akiwa kama mama watoto wawili mapacha yamekuwa ya aina yake na anayafurahia kila sekunde.

“Nimejifunza kuwa mvumilivu, nimejifunza upendo ambao sijawahi kujisikia kabla. Jinsi unavyompenda mtoto ni tofauti ambavyo unaweza kumpenda mtu yoyote yule katika maisha yako,” alisema.

Katika hatua nyingine Miss Tanzania huyo wa zamani alisema hakuna uwezekano wowote wa yeye kurejea tena kwenye muziki.

“Kwa bahati nzuri sana baada ya kufanya uamuzi wa kutokuwa kwenye muziki, niliweza kupata kitu kingine ambacho kimeuteka moyo wangu. Kufanya interior design kunanifurahisha kuliko hata muziki. Nafurahi sana kujua kwamba kuna watu wangependa kunisikia ama kusikia nikiimba lakini nafikiri moyo wangu umehamia kwenye sanaa nyingine.”

Mtazame zaidi hapo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents