Kabendera kukutana na upande wa mashitaka

Hatima ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Mwanahabari, Erick Kabendera itajulikana February 17, 2020 baada ya upande wa mashitaka kuomba kuzungumza na Kabendera kwa siri kwa ajili ya kuingia nae makubaliano.

Hatua hiyo inakuja wiki chache baada ya Kabendera kuomba kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP) kwa ajili ya maelewano.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega kuwa kwa muda mrefu kulikuwa na mchakato wa maelewano baina ya Mshitakiwa na DPP, hivyo wapo katika hatua ya mwisho “tunaomba kuzungumza na mshitakiwa kwa sababu tayari tulishazungumza na Mawakili wake”

Hakimu Mtega amesema kutokana na ombi hilo la upande wa mashitaka anawakubalia, hivyo anaahirisha kesi hiyo hadi Februari 17, 2020.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW