Tupo Nawe

Kabendera yuko huru, atakiwa kulipa faini ya mil 273 alipa mil 100 kwenye akauti ya Serikali, Nyingine baada ya miezi 6 – Video

Kabendera yuko huru, atakiwa kulipa faini ya mil 273 alipa mil 100 kwenye akauti ya Serikali, Nyingine baada ya miezi 6 - Video

Serikali ya Tanzania imemuondolewa mwandishi wa habari Erick Kabendera shtaka moja la kuongoza genge la uhalifu. Mwandishi wa habari za kiuchunguzi, Erick Kabendera yuko njiani kuachiwa huru saa yoyote kuanzia sasa.

leo Februari 24, 2020, ameondolewa shtaka moja la kujihusisha na genge la uhalifu,.Hatua hiyo ya mwenendo wa kesi inayomkabili inafuatia kukamilika kwa mazungumzo na makubaliano baina yake na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), hii leo.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu.

Mashtaka hayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 milioni. Kwa uamuzi huo sasa Kabendera atakuwa na mashtaka mawili ambayo ni kukwepa kodi na kutakatisha fedha.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Februari 24, 2020 na wakili wa Serikali mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Janeth Mtega wakati akimsomea mashtaka mshtakiwa huyo. Kabendera amekiri mashtaka yake mawili.

Mahakama ya Kisutu imemuhukumu Mwanahabari Erick Kabendera kulipa fidia na faini ya Sh. Mil 273 baada ya kukiri makosa ya utakatishaji fedha na kukwepa kodi, tayari ameshaingiza Tsh. Mil 100 kwenye akaunti ya Serikali na ameachiwa huru huku akitakiwa kulipa fedha iliyobaki ndani ya miezi sita.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega baada ya Kabendera kusota rumande kwa takribani miezi sita.

Chanzo Mwananhi digital

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW