Michezo

Kabla Super Cup dhidi ya Liverpool, Lampard awaonya vijana wake, awakumbusha kilichowapata mbele ya United 

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amewaonya wachezaji wake kuwa kamwe hatohitaji kuombwa msamaha hapo kesho siku ya Jumatano kama watapoteza mbele ya Liverpool mchezo wa fainali ya Super Cup.

Frank Lampard expects his players to deliver a strong performance in the Super Cup final

Lampard ameyasema hayo wakati akiwa na kumbukumbu ya kupokea kipigo kizito cha mabao 4 – 0 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wake wa kwanza wa Premier League.

Kutokana na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Europa League msimu uliyopita Chelsea itakabiliana na mshindi wa taji la Champions League, Liverpool hapo kesho huko Istanbul.

“Tunakwenda kukabiliana na kikosi bora cha Liverpool katika fainali,” Lampard ameiyambia tovuti ya uefa.com.

“Kila mchezaji atapaswa kuwa na uelewa juu ya umuhimu wa  huu mchezo ndani ya klabu hii, tumewapa kila kitu kwasababu utakuwa mgumu.”

“Itakuwa mechi ngumu, lakini hatuwezi kuukimbia uwanja, tulishafanya hivyo, tulishakosa nafasi kama hii, hatutoruhusu kuombana msamaha wenyewe kwa wenyewe.”

Lampard mwenye umri wa miaka 41, akiwa kocha mpya wa Chelsea kwa mara ya kwanza anakutana na adhabu ya kutoruhusiwa kufanya usajili kwa misimu miwili huku akishuhudia nyota wake Eden Hazard akitimkia Madrid.

Wakati wakijipanga kwaajili ya kombe la Super Cup, Loampard ni kama mwenye mkosi kwani anakumbukwa akilikosa taji hili mwaka 1998, kwa misimu miwili mfululizo wakati akiwa mchezaji Lampard. “Tunapaswa kuwa tayari.”

“Hili ni taji ambalo kama klabu tunahitaji kushinda, binafsi sikuwahi kulitwaa na wachezaji wengi pale hawajawahi kushinda hivyo tunapaswa kufanya kila tuwezalo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents