Michezo

Kabla ya kuivaa Valencia Champions League, Mourinho asisitiza wapo wachezaji wanaompa ushirikiano

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose  Mourinho licha ya kuripotiwa kutokuwa na maelewano mazuri na wachezaji wake amesema kuwa wapo ambao anaoelewana nao na kujitolea zaidi.

The Portuguese  questioned some of his players' motivation and effort during their recent run

Maneno ya Mourinho yanakuja wakati akitarajia kushuka uwanjani hapo kesho siku ya Jumanne kukabiliana na Valencia mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya.

Mreno huyo amekuwa kwenye kipindi kigumu na kukosa kujiamini tangu United kushindwa kufanya vizuri mwanzoni mwa msimu huu na hata kushindwa kuonyesha makali mbele ya Derby County na West Ham huku akihusishwa kutimuliwa kama meneja wa mashetani hao wekundu.

Mourinho amesisitiza kuwa wapo baadhi ya wachezaji anao elewana nao ma kumuamini huku wakimjali zaidi ya hao wengine.

Alipoulizwa na waandishi wa habari mchana wa leo juu na fasi yake kama ameshaongea na makamu mwenyekiti wa United, Ed Woodward amesema kuwa hayo ni mambo binafsi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents