Michezo

Kabla ya Manchester United kuikabili Chelsea fainali ya FA, Mourinho atangaza amani na Conte

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa vita yake ya maneno na Kocha Mkuu wa Chelsea, Antonio Conte itakwisha kwenye mchezo wao fainali kombe la FA utakao pigwa hapo kesho siku ya Jumamosi.

Vita ya maneno kati ya makocha hawa wawili ilianza kushika kasi msimu uliyopita baada ya Mourinho kumtuhumu Muitalia huyo, Conte kuwa alikuwa akisherehekea kwa dharau wakati Chelsea ilipoibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4 – 0 dhidi ya United dimba la Stamford Bridge.

 

 

Kupitia mahojiano yake na gazeti la Ureno, Mourinho amesema kuwa mahusiano yake na Conte yapo vizuri.

”Tupo vizuri kabisa tunasalimiana na kupeana mikono maana tulisha choshwa na hayo mambo. Baada ya mechi tulipokuwa Manchester nilimualika kwenye ofisi yangu na kuzungumza.” amesema Mourinho

Vijembe vikaendelea tena msimu huu baada ya Conte kutumia maneno ya Kiitaliano ya “demenza senile” akimaanisha Mourinho anamatatizo ya akili jambo lililomfanya meneja huyo wa United kumjibu kwa kumuambia nae alifungiwa na klabu yake ya zamani ya Siena na kisha baadae kuachiliwa huru.

Bosi huyo wa United amesema kuwa kwa sasa wameelewana na hakuna kitu chochote cha tofauti kitaripotiwa kati yao watakapo kutana hapo kesho kwenye dimba la Wembley.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents