Michezo

Kabla ya Mbao, Azam FC kuivaa Mabatini Kombaini

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kukipiga dhidi ya Mabatini Kombaini katika mchezo wa kirafiki unaotarajia kufanyika Uwanja wa Alliance kesho Jumatano majira ya saa 10.00 alasiri.

Kikosi cha Azam FC kipo mkoani Mwanza tokea juzi, kikifanya maandalizi ya kuikabili Mbao, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaotarajia kufanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu uliopita wanaodhaminiwa na Maji Safi ya Uhai Drinking Water, Benki Bora ya NMB na Tradegents, wanatarajia kuutumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wao na Mbao.

Hadi hivi wachezaji wote wa Azam FC wako fiti, isipokuwa kipa Razak Abalora, anayesumbuliwa na Malaria, ambaye leo ameanza mazoezi mapesi asubuhi katika Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa Mwanza.

Kueleka mchezo wa Mbao, Azam FC imeonekana kuwa kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa ni miongoni mwa timu nne zilizokaa kileleni zote zikiwa na pointi 12, zingine zilizojuu yake zikiwa ni Simba SC, Yanga SC na Mtibwa Sugar, ambazo ziko juu yake kwa idadi ya mabao ya kufunga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents