Michezo

Kabla ya Octoba 28,hizi ndiyo salamu za Simba SC kwa Yanga SC

Ligi kuu soka Tanzania Bara imeendelea hii leo kwa michezo sita kupigwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini.

Katika michezo hiyo timu ya soka ya Simba SC ikiwa nyumbani katika Uwanja wa Uhuru imechomoza na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya klabu ya Njombe Mji.

Wafungaji katika mchezo huo ni Emmanuel Okwi akiwa amefunga bao moja na kufikisha jumla ya nane msimu huu na Mzamiru Yassin akifunga mawili huku la mwisho likihitimishwa na Laudit Mavugo.

Mpaka sasa simba SC inaongoza katika msimamo wa ligi kwa kuwa na jumla ya pointi 15 ikifuatiwa na Yanga SC yenye alama 12 kabla ya mchezo wake wa kesho siku ya Jumapili dhidi ya Stand United huku wawili hao wakitarajiwa kukutana Octoba 28.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa hii leo kule Mtwara, Ndanda FC imebanwa mbavu na Singida United na kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na huko Mwanza, Azam FC imeikazia Mbao FC na kulazimisha suluhu, Iringa, Lipuli imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Majimaji FC, Manungu Morogoro, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prison.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents