Michezo

Kabla ya pambano lao kati ya Wilder na Breazeale leo usiku, kauli ya Wilder yakusema anatamani kufanya mauaji ulingoni yazua ngumzo

Deontay Wilder anahatarisha historia yake katika ulimwengu wa ndondi kufuatia matamshi yake ya kutekeleza mauaji katika ukumbi wa ndondi.

Kwa mujibu wa BBC. Wilder ambaye ni bingwa wa ukanda wa WBC katika uzani mzito zaidi duniani amekosolewa kwa kudai kwamba atamuua mpinzani wake- baada ya kusema kwamba atahakikisha kuwa ameua katika rekodi yake ya mapigano.

Lakini mkufunzi wa mpinzani wake Dominic Brazeale -Virgil Hunter alisema kuwa hakufurahishwa na matamshi hayo ya bingwa huyo.”

Anahitaji kujiuliza iwapo hilo ndio lengo lake pekee, je hii ndio historia ninayopaswa kuwacha nyuma? Nadhini hicho ni kitu ambacho Deontay anahitaji kukabiliana nacho katika nafsi yake- Hunter aliambia BBC Sport mjini New York.

”Je huu ndio mfano ninaotaka kuonyesha , nadhani baadaye anahitaji kuomba msamaha”.

Bingwa wa zamani katika uzini mzito Frank Bruno alikosa matamshi ya Wilder katika mtandao wa Twitter, huku aliyekuwa bingwa mara mbili katika uzani huo Nigel Benn akisema kuwa ,matamshi hayo yalikuwa ya aibu katika ndondi.

Bingwa huyo wa ukanda wa WBC alitoa matamshi kama hayo hapo awali kuyarejelea tena katika vyombo vya habari pamoja na vipindi vya majadiliano nchini Marekani wiki hii.

Raia huyo wa Marekani alitetea matamshi yake siku ya Jumanne na alipoulizwa kuhusu swala hilo na BBC Sport siku ya Jumatano, alisema: Sijutii chochote ninachosema. napenda ninachosema na kile ninachofanya.

Hunter ambaye pia mkufunzi wa masumbwi wa bondia Muingereza Amir Khan aliongezea: Ni njia ya makosa kutumia maneneo kama hayo kupromoti mchuano. Nimesikitishwa

Wilder na BreazealeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWilder (kushoto) ameshinda mara 40 na kupata sare moja katika mapigano yake 41

”Yuko juu ya ulimwengu kwa kutumia mikono yake na sasa anafanya makosa kutoa taarifa kama hizo, hiyo inawafanya watu kuogopa. Ni matamshi yasiofaa”.

Aliyekuwa bondia wa zamani katika uzani mzito Tony Bellew na promota Eddie Hearn pia wamekosoa matamshi hayo ya Wilder hapo mbeleni.

Raia huyo wa Marekani ni mpinzani wa Brazeale ambapo wawili hao karibia wapigane katika hoteli moja mwaka 2017.

Brazeale alisema mamake Wilder alimpiga mbele ya mkewe na mwanawe. Alipoulizwa kuhusu matamshi ya Wilder, Brazeale aliambia BBC Sport: Ni makosa unadhani ni nani anayeweza kusema mambo ya kipuuzi kama hayo. ”Hufai kusema hivyo kuhusu mpinzani wako. Ni muhimu kuwa na uanaspoti ndani yako. Unafaa kuwa mtaalam katika mchezo huu”.

”Usingependelea mtu kuumia katika pigano. katika pigano hili tuna sababu za kibinafsi na malengo lakini iwapo ataumia ni sawa. lakini siwezi kuomba kifo hapana siwezi”. Brazeale amepoteza pigano moja kati ya mapigano 21- ikiwa ni knockout ya raundi ya saba dhidi ya Anthony Joshua 2016. Raia huyo wa Marekani atajaribu kumshinda kwa mara ya kwanza Wilder-ambaye ameshinda mara 40 na kupata sare moja katika mapigano 41.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents