Burudani ya Michezo Live

Kabwili adai Simba walimtaka aisaliti Yanga ”Wameniambia wananipa IST”(+Video)

Mlinda mlango wa klabu ya Yanga, Ramadhan Kabwili amedai kuwa aliwahi kufuatwa na Simba wakimtaka atafute kadi ili asicheze mchezo wa watani wa jadi na watampatia gari aina ya IST.

Kabwili amesema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Kipenga Xtra cha East Africa Radio, Jumatatu, Januari 27, 2020 ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea wakati Yanga ikiwa na kocha Mwinyi Zahera.

”Tunakupa kadi na ufunguo, vitu vyote hivyo vitakuwa vya kwako na tuna kusainisha kabla ya mechi na JKT Tanzania. Ili uweze kupata kadi tatu za njano usihusike na mchezo wa kwetu.” Amesema Kabwili.

Ramadhan Kabwili ameongeza kuwa ”Ili aweze kuhusika Klaus Kindoki  maana wanaamini akihusika Kindoki wangeweza kupata mabao kirahisi. Ni kitu ambacho kilinifanya hadi ni badili laini, kwa sababu nilikuwa na laini kama tatu. Kwa sasa siitumi kabisa niliitupa.”

Mchezaji huyo amedai kuwa siku hiyo Yanga ilikuwa inaelekea kucheza na JKT Tanzania na yeye alikuwa tayari ana kadi mbili za njano, hivyo Simba walimfuata na kumuambia kuwa atafute kadi moja ya njano ili akose mchezo uliokuwa unafuatia wa watani wa jadi huku wakimuahidi kumpa IST mpya, wakiamini kuwa angekaa Klaus Kindoki golini wangemfunga kirahisi.

Katika mchezo huo dhidi ya JKT Tanzania, Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1 – 0 ambapo Ramadhan Kabwili ndiye alikuwa golikipa wa Yanga siku hiyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW