Kaduguda kumwaga mshiko akishukuru kusimamishwa

KadugudaKlabu ya Simba ikiwa imetangaza kumsimamisha uongozi kwa muda usiojulikana Katibu Mkuu wao Mwina Kaduguda, kiongozi huyo amesema atamwaga mshiko kwa uongozi wa Simba na kwenye kundi la vibopa wa klabu hiyo, ikiwa ni shukrani kwa hatua waliyochukua ya kumsimamisha

Kaduguda


 


Klabu ya Simba ikiwa imetangaza kumsimamisha uongozi kwa muda usiojulikana Katibu Mkuu wao almaarufu kwa jina la Mwina Kaduguda kwa kile kilichodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu, kiongozi huyo amesema atamwaga mshiko kwa uongozi wa Simba na kwenye kundi la vibopa wa klabu hiyo maarufu kama Friends of Simba, ikiwa ni shukrani kwa hatua waliyochukua ya kumsimamisha.


 


Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ilikutana hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika kikao cha dharura kilichokuwa kikimjadili Kaduguda kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo kutoa kauli iliyomuudhi sana tajiri aliyekuwa akimlipa mshahara Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mserbia Milovan Cirkovic.


 


Akizungumza mara tu baada ya kikao hicho Dar es Salaam, Katibu Mwenezi wa klabu hiyo, Said Rubeya, alisema wamefikia uamuzi wa kumsimamisha hadi hapo Mkutano Mkuu wa Simba utakapofanyika na kuamua vinginevyo.


 


“Tunashukuru tumemaliza kikao muda huu na tumefikia uamuzi wa kumsimamisha Kaduguda katika wadhifa wake hadi hapo Mkutano Mkuu utakapofanyika kutokana na tuhuma mbalimbali,” alisema Rubeya.


 


Alisema mkutano huo ndio wenye mamlaka ya kuamua chochote na kwamba wametekeleza majukumu yao ya kikatiba, lakini Kaduguda alipoulizwa alisema kama ni kweli amesimamishwa na itakuwa faraja kwake, na kudai kila kiongozi wa Simba atamgawia sh. 200 na wote wanaounda kundi la Friends of Simba pia atawapa kiasi hicho cha fedha kila mmoja.


 


“Sawa ngoja nisubiri hiyo barua, lakini ninachojua kikao kilimalizika salama juzi(Jumapili), tutakutana tena Jumapili, hayo mambo mengine yananishangaza,” alisema Kaduguda.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents