Tupo Nawe

Kaimu Balozi wa Marekani, Dkt. Patterson awafunda wanafunzi wa Jangwani Girls’ (+video)

Leo katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani Tanzania, Dkt. Inmi Patterson ametembelea shule ya Wasichana ya Sekondari ya Jangwani iliyopo jijini Dar Es Salaam.

Akiwa shuleni hapo, Dkt. Patterson alizindua mashine maalumu za kuuzia Taulo za Kike “Sanitary Pads” mashuleni, ambazo zitauzwa kwa bei rahisi ili kuwasaidia wanafunzi kujistiri kipindi cha cha hedhi bila kubughuzi mahudhurio yao darasani.

Mashine hizo zimetengenezwa na kikundi cha Wajasiriamali kiitwacho Sauti ya Binti, ambapo Pads na mashine zimetengenezwa hapa nchini.

Kwa upande mwingine, Balozi Patterson amewafunda wanafunzi hao kuthamini miili yao na kujitambua ili waweze kufikia malengo ya usawa wa kijinsia.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW