Habari

Kairuki akanusha tetesi kuwa serikali itaanza kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angela Kairuki amekanusha tetesi kuwa serikali itaanza kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao.

kairuki

Amelazimika kuzikanusha taarifa alizoziita za uongo kupitia akaunti yake ya Twitter.

“Kuna taarifa ya uongo inayosambazwa mtandaoni kwamba “kutakuwa na zoezi la kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao, Ipuuzieni,” ameandika.

twitter

“Si dhamira wala desturi ya Serikali yetu kuingilia maisha binafsi ya watumishi wa umma hususan matumizi ya mishahara yao.Puuzieni uzushi huo,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents